Mkurugenzi wa Tume Huru ya Uchaguzi INEC, Ramadhan Kailimakazi akifungua semina ya maafisa habari wa mikoa ba halmashauri za wilaya kuhusu uboreshaji wa daftari la wapiga kura.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu kwa Mpiga Kura Tume Huru ya Uchaguzi!Bi. Giveness Aswile akifafanua jambo katika semina hiyo.
TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imesema kuwa katika kuhakikisha inakwenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia ikiwa ni pamoja na kurahisisha zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura imeboresha mfumo wa uandikishaji.
Imesema fumo huo ulioboreshwa kwa mara ya kwanza utamuonyesha mpiga kura aliyekuwepo kwenye daftari kuanzisha mchakato wa kuboresha hama kuhamisha taarifa zake kwa kutumia simu ya mkononi au kompyuta na baadae atakamilisha mambo mengine yanayohitajika ikiwemo na kupiga picha.
Hayo yamebainishwa hayo leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Tume Huru ya Uchaguzi INEC, Ramadhan Kailima wakati akifungua mkutano wa tume hiyo na Maofisa Habari wa Mikoa na Halmashauri za Tanzania Bara kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura.
Anasema maofisa habari wa mikoa na halmashauri wanajukumu la kuwaelimisha na kuhabarisha wananchi wakiwemo walemavu ili kupata uelewa wa kutosha kuhusu uboreshaji na hatimaye wajitokeze kwa wingi kujiandikisha.
“Lengo la kukutana nanyi ni kuendelea kuwakumbusha kuwa mnajukumu kubwa la kuwahabarisha umma ili waweze kujitokeza kwa wingi katika zoezi hili la uboreshaji wa daftari ambalo litaanza Julai Mosi mwaka huu.
“Aidha nawaomba wadau mbalimbali wa uchaguzi wazingatie sheria za Uchaguzi, kanuni za uboreshaji na maelekezo ya tume, kwa upande wa maofisa wa tume watazingatia Sheria za uchaguzi katika zoezi hili,” anasema
Kailimia pia amewataka waandishi wa habari kupinga aina yoyote ile ya uposhwaji ili kurahisisha kazi hiyo kufanyika kwa uzuri na ufanisi mkubwa.
Anasema INEC inatarajia kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa maofisa habari hao ambao wanafanyakazi kubwa ya kuhabarisha umma katika mikoa na halmashauri wanazofanyia kazi.