Matukio mbalimbali pichani yakimuonesha Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura akiwa na ujumbe wake alioambatana nao wakiwa na Mhe. Lt Gen Mathew Edward Mkingule, ambaye ni Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Zambia wakati walipomtembelea ofisini kwake Lusaka Zambia Juni 14, 2024.
IGP Wambura yupo nchini Zambia ambapo jana alikabidhiwa uenyekiti wa Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO) kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Zambia IGP Graphel Musamba ambaye amemaliza muda wake wa kuliongoza shirikisho hilo.