Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania TPHPA imefanikiwa kuwa Mshindi wa Tuzo kundi la Taasisi zisizo za kibiashara zilizofanya mageuzi makubwa kiuendeshaji.
Taasisi ya TPHPA imeitikia kwa vitendo maagizo ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha ufanisi wa taasisi za umma na taasisi za serikali kupitia mwongozo wa Msajili wa Hazina. Ndani ya Wizara ya Kilimo, TPHPA ililenga kuboresha katika maeneo yafuatayo
Akizungumza na Fullshangweblog Ikulu jijini Dar es Salaam maa baada ya kupokea tuzo hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya TPHPA Profesa Andrew Temu wakati taasisi za Umma zilipokabidhi Gawio kwa Rais Samia Suluhu Hassan.
Profesa Andrew Temu amesema TPHPA Ililenga maboresha ya miundombinu, kuanzia na mageuzi katika Bodi na ngazi za Usimamizi, kuingiza na kuhamasisha utendaji wa wafanyakazi kutoka idara za wizara na taasisi nyingine husika zinazohusika na afya ya mimea
Ameongeza kuwa Taasisi hiyo iliwekeza na kujenga mifumo ya kidijitali kusimamia utawala wa mamlaka, kuboresha utendaji, na kuratibu vitengo tofauti vya Mamlaka, kusimamia shughuli za afya ya mimea na udhibiti wa viuadudu, kufuatilia na kudhibiti milipuko ya wadudu wa mimea (magonjwa na wadudu wanaoharibu mazao kama vile nzige, minyoo wa jeshi, nzi wa matunda, na panya) katika Tanzania bara na Zanzibar
Amesema kuwa ilikuwa ni Kuboresha vifaa, ikiwa ni pamoja na zana za maabara, magari na pikipiki, kompyuta na vifaa vingine vya nje, ndege zisizo na rubani, mitandao ya kidijitali (mtandao wa intaneti), na vifaa vya upelelezi kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa na wadudu wanaoharibu mazao, na kuboresha na kuwezesha masoko ya kilimo ya kimataifa.
Ameongeza kuwa Kupitia ada mbalimbali za huduma za afya ya mimea na udhibiti wa viuadudu ili kuhakikisha kuwa wadau wako tayari na wana nia ya kulipa mamlaka imefanikiwa kufanya maboresho
Ya mifumo ya ICT kwa ajili ya ukusanyaji wa mapato katika vituo 36 vya mpakani, ofisi 7 za kikanda, na katika maabara, vitengo, na vituo mbalimbali vya Mamlaka kote nchini.
Bodi ya Wakurugenzi na Usimamizi wa Mamlaka imeandaa mkakati wa utekelezaji wa majukumu yao kwa kuzingatia Mkataba wa Kimataifa wa Ulinzi wa Mimea (IPPC), ambao Tanzania iliridhia mwaka 2005. Mkakati huu unazingatia vipaumbele vya Wizara ya Kilimo, ikiwa ni pamoja.
Profesa Temu amesema wamefanikiwa Kuongeza uzalishaji , Kuunda ajira, hasa kwa vijana na wanawake
Kuimarisha masoko ya kilimo
Pia usalama wa chakula nchini
Umeimarishwa amnapo pia kumekuwa na ushirikiano kwa
Kutumia ICT kwa na kuwa na ufanisi.
Yote hayo yamepelekea pia ukusanyaji wa maduhuli kuongezeka na hivyo basi gawio la asilimia 15 ambalo serikali imepokea
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Profesa Andrew Temu Mwenyekiti wa Bodi ya TPHPA kushoto na Prof. J Ndunguru Mkurugenzi Mkuu TPHPA.
Profesa Andrew Temu Mwenyekiti wa Bodi ya TPHPA kushoto na Prof. J Ndunguru Mkurugenzi Mkuu TPHPATPHPA wakiwa na tuzo yao.
Profesa Andrew Temu Mwenyekiti wa Bodi ya TPHPA kushoto na Prof. J Ndunguru Mkurugenzi Mkuu TPHPATPHPA walipozi kwa picha.