Mkurugenzi wa Uchaguzi, Kailima Ramadhan akiwasilisha mada katika kikao hicho kati ya wahariri wa vyombo vya habari na Tume huru ya Uchaguzi kilichofanyika leo Mlimani City jijini Dar es Salaam.
……………….
TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imesema idadi ya Vituo vya Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura imeongezeka kutoka 37,814 hadi 40,126 sawa na ongezeko la Vituo 2312.
Akizungumza katika Mkutano na Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Kailima Ramadhan, alisema Tume tayari imekamilisha maandalizi yote.
Alisema katika Vituo hivyo 39,709 vipo Tanzania Bara na vingine 417 vipo Zanzibar.
“Hili ni ongezeko la Vituo 2,312 ukilinganisha na Vituo 37,814 vilivyotumika 2019/2020,”alisema Kailima.
Aidha, Kailima alisema kwa kudhingatia matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022; Wapiga kura wapya 5,586,433 wanatarajiwa kuandikishwa ambao ni sawa na asilimia 18.7 ya Wapiga kura 29,754,699 ya waliopo katika Daftari baada ya uboreshaji uliyofanyika kwenye mwaka 2019/20.
Pia Wapiga kura 4,369, 531 wanatarajiwa kuboresha Taarifa zao na wengine 594,494 wataondelewa kwenye Daftari kutokana na Kukosa sifa za Kuendeleza kuwepo kwenye Daftari hilo.
Kwa mujibu wa Tume hiyo, baada ya uboreshaji huo inatarajiwa kuwa Daftari litakuwa na jumla ya Wapiga kura 34,746,638.
Akizungumzia utaratibu wa kuandikisha wafungwa wa gereza/Wanafunzi wa vyuo vya mafunzo na mahabusu, Kailima alisema Kanuni ya 15(2)(c), ya Kanuni za Uboreshaji wa Dafta hilo la Wapiga kura za Mwaka2024.
“Tume imeweka Utaratibu wa kuwezesha wafungwa/Wanafunzi waliohukumiwa kifungo cha chini ya miezi sita na mahabusu kuandikishwa kuwa Wapiga kura,”alisema Kailima.
Aidha, Tanzania Bara kuna Vituo vya kuandikisha Wapiga kuta 130 vilivyopo katika magereza na kwa upande wa Zanzibar kuna Vituo 10 vilivyopo kwenye vyuo vya Mafunzo.
Awali Mwenyekiti wa INEC, Jaji (Rufaa), Jacobs Mwambegele, aliviasa vyombo vya habari kuwashauri wote watakaodhani kuna changamoto, watumie njia zilizopo kwenye sheria.
“Vyombo vya habari vinaweza kuwakumbusha Wadau wenye malalamiko kutumia mifumo sahihi ya uwasilishaji na kushughulikiwa changamoto husika,”
Picha zikionesha wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakishiriki katika kikao kazi hicho.