Mkurugenzi wa kampuni ya kitalii ya Pamoja Afrika iliyopo Karatu,Asheri Kiisay akizungumza na wateja walipotembelea banda lao kwa ajili ya kupata maelezo ya huduma wanazotoa.
…………..
Happy Lazaro, Arusha.
Watanzania wametakiwa kuwa na utamaduni wa kutembelea hifadhi za kitalii zinazotuzunguka ili kutangaza utalii wa ndani badala ya kuachia wageni kutoka nje kuja kutangaza utalii hapa kwetu.
Aidha amesema kuwa ,ni vizuri wakajenga utamaduni wa kuvienzi vya kwetu kwani vivutio mbalimbali vya utalii ni vya kwetu na vinatuhusu sisi wenyewe ,hivyo ni lazima tujenge utaratibu wa kutembelea hifadhi mbalimbali na kutangaza vivutio vilivyopo.
Hayo yamesemwa mkoani Arusha na Mkurugenzi wa kampuni ya kitalii ya Pamoja Afrika iliyopo Karatu,Asheri Kiisay ambapo amesema wataendelea kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii katika nchi mbalimbali huku lengo likiwa kumuunga mkono Rais Samia .
Amesema kuwa, endapo sisi kama watanzania tutajenga utamaduni wa kutembelea hifadhi mbalimbali itasaidia sana sisi wenyewe kuwa mabalozi wazuri kwa ajili ya kutangaza vivutio hivyo na hivyo kuendelea kuwashawishi wafadhili mbalimbali kutembelea.
Aidha amesema kuwa,kupitia kampuni hiyo wamekuwa wakitangaza vivutio mbalimbali vya utalii kwa watalii wanaofika katika eneo hilo kutokana na mandhari nzuri iliyopo inayovutia na kuwafanya wengi wao kuendelea kufika eneo hilo.
Ameongeza kuwa, watalii wanaweza kujionea hoteli inayotembea kufuata wanyama wanaohama kutoka Tanzania kwenda Masai Mara .
“Tanzania ni nchi nzuri sana na tumejionea namna ambavyo utalii umezidi kushika kasi baada ya Rais Samia kutangaza utalii kupitia filamu yake ya The Royal Tour kwani ametusaidia sana kufungua nchi na kuturahisishia kupata watalii wanaotoka nchi mbalimbali kuja kujionea vivutio vyetu.”amesema .
Amesema kuwa,watalii wanapokuwa kwenye hotel hiyo wanaweza kufanya utalii wakati wa usiku kwani ni mida ambayo unaweza kuona wanyama kwa karibu zaidi .
Aidha akizungumzia mafanikio makubwa waliyoyapata katika maonyesho hayo ambayo hufanyika kila mwaka ni pamoja na kupata idadi kubwa ya wanunuzi wapya kwani kupitia filamu ya The Royal Tour ya Rais Samia imesaidia sana watalii kuendelea kufurika hapa nchini kwa ajili ya kujionea vivutio mbalimbali .
Hata hivyo amewataka watalii mbalimbali.ndani na nje ya nchi kujitokeza kwa wingi katika katika maeneo hiyo ili waweze kujifunza maswala mbalimbali ya vitutio.