Wafanyabiashara wa Kijiji cha Ikumbilo kilichopo Kata ya Chitete Wilaya ya Ileje Mkoa wa Songwe wametakiwa kuacha tabia ya kutumia muda mwingi kutafuta pesa bali wanatakiwa kutenga muda wao kutimiza wajibu wao katika utoaji malezi bora kwa watoto wao.
Wito huo umetolewa Juni 10, 2024 na Polisi Kata ya Chitete Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Nsajigwa Mwajeka alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara hao ambapo aliwataka kuacha tabia ya kuwaachia watoto watu wasiowafahamu pindi wawapo kwenye biashara zao ili kuweza kuzuia watoto kuibiwa au kufanyiwa ukatili.
Sambamba na hilo, Mkaguzi Mwajeka amewataka wananchi hao kupiga vita dhidi ya matukio yote ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia na yeyote atakaetendewa afike katika kituo cha Polisi kwa hatua zaidi ikiwa ni pamoja na wahusika kufikishwa mahakamani.WhatsApp Image 2024-06-08 at 03.57.08_8c76d645.jpgWhatsApp Image 2024-06-08 at 03.57.08_4820ff7c.jpgWhatsApp Image 2024-06-08 at 03.57.09_6fea76b3.jpg