Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Italia Marco Lombardi ambaye amemaliza mudawake nchini, katika Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni Jijini Dar es Salaam, Juni 09, 2024 (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
………………….
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Juni 09, 2024 amefanya mazungumzo na Balozi wa Italia Nchini Tanzania Balozi Marco Lombardi ambaye amemaliza muda wake, Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es Es Salaam.
Katika mazungumzo hayo Waziri Mkuu amesema Tanzania itaendelea kuwa mshirika muhimu na wa kimkakati wa nchi ya Italia.
Kwa upande wake Balozi Lombardi amesema licha ya kumaliza muda wake kama Balozi wa Italia nchini Tanzania, bado ataendelea kuisemea Tanzania na kuwa mhamasishaji wa fursa zilizopo nchini nchini.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Italia Marco Lombardi ambaye amemaliza muda wake nchini, katika Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni Jijini Dar es Salaam, Juni 09, 2024 (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)