Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule ameshiriki uzinduzi wa Taasisi ya Nguvumoja Youth Power inayojihusisha na kuinua vijana kwa kuwapa mitaji na kutoa elimu kwa vijana leo tarehe 08 June 2024 katika ukumbi wa Chimwanga Jijini Dodoma
Akitoa salamu za Mkoa kwa vijana walioshiriki uzinduzi huo wenye lengo la kuwawezesha vijana kujiajiri, kusaidia vijana zaidi ya Elfu mmoja ndani ya mwaka 2024, Mhe. Senyamule amesema;
“Serikali inatekeleza mipango mingi ya vijana kwa kuwapa mikopo mbalimbali na ndio maana Kuna mikopo ya 10% kutoka kwenye Halmashauri ambayo hupewa vijana waliojisajili kwenye kikundi chebye vigezo stahiki ili weweze kujikwamua kiuchumi”
“Vijana changamkieni fursa zinazokuja na kuzifanyia kazi ili kuendeleza nguvu kazi kwa vijana maana Taifa linawategemea sana vijana” Amesema Senyamule.
Vilevile katika uzinduzi huo ambao Mgeni Rasmi alitarajia kuwa Mhe.Deogratus Ndejembi Waziri wa kazi, ajira na watu wenye ulemavu, aliwakilishwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Patrobas Katambi