AMISHNA Jenerali wa Jeshi la Magereza, Mzee Ramadhani Nyamka ameondoka mapema LEO Juni 9, 2024 kuelekea katika Mji wa Makka nchini Saudi Arabia kwenda kutekeleza ibada ya Hijja ambayo ni nguzo ya Tano katika Uislamu.
Aidha, akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. JK Nyerere, Terminal One amekutana na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuberi, Sheikh Kizenga na aliyekuwa Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam, Sheikh Alhad Mussa ambaye wataambatana kwenda kutekeleza Ibada hiyo ya Hijja.