Mkurugenzi wa Taasisi ya Chukula na Lishe Tanzania (TFNC) Dkt. Germana Leyna akizungumza katika kikoa wakati wafadhili wa mradi wa majaribio wa kutengeneza bidhaa aina ya asusa yenye lengo la kuwasaidia watoto wenye umri kuanzia miaka 6 hadi 19 ambao wana upungufu wa damu kutoka Chuo Kikuu cha Tsing Hua nchini China walipotembelea leo Juni 7, 2024 Maabara ya TFNC iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia utekelezaji wa mradi huo.
Profesa Al Zhao kutoka Chuo Kikuu cha Tsing Hua (kushoto) akimkabidhi Zawadi Mkurugenzi wa Taasisi ya Chukula na Lishe Tanzania (TFNC) Dkt. Germana Leyna.
Mtafiti Mkuu wa Taasisi ya Chukula na Lishe Tanzania Dkt. Anselm Moshi akiwasilisha taarifa ya utekelezajiwa wa mradi wa majaribio wa kutengeneza bidhaa aina ya asusa yenye lengo la kuwasaidia watoto wenye umri kuanzia miaka 6 hadi 19 ambao wana upungufu wa damu.
Watumishi wa Taasisi ya Chukula na Lishe Tanzania (TFNC) akiwa katika picha ya pamoja na wadao wao kuoka Chuo Kikuu cha Tsing Hua kutoka nchini China.
Picha za matukio mbalimbali
………
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Taasisi ya Chukula na Lishe Tanzania (TFNC) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Tsing Hua kutoka nchini China wapo katika utekelezaji wa mradi wa majaribio wa kutengeneza bidhaa aina ya asusa yenye lengo la kuwasaidia watoto wenye umri kuanzia miaka 6 hadi 19 ambapo imebainika zaidi ya asilimia 50 wana upungufu wa damu.
Akizungumza leo Juni 7, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wadau kutoka Chuo Kikuu cha Tsing Hua walipotembelea Maabara ya TFNC iliyopo Mikocheni kwa ajili ya kuangalia utekelezaji wa mradi huo wa majaribio, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chukula na Lishe Tanzania Dkt. Germana Leyna, amesema kuwa lengo la mradi ni kutengeneza asusa ambayo inaweza kutatua changamoto ambazo wanapitia vijana balehe ya ukosefu wa afua za lishe.
Dkt. Leyna amesema kuwa kwa mujibu wa utafiti uliofanyika mwaka 2009 na 2021 wa hali ya ugonjwa wa malaria na watoto waliopo shuleni wanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa damu.
“Wataalamu wameweza kutengeneza formulation ambayo itatumia maharage ambayo yamerutubishwa na zinc pamoja na madini chuma, mahindi ya njano kwa ajili ya kutengeneza biscut, kwa sasa tupo katika hatua ya awali ya kupeleka mashuleni ili kupata mrejesho” amesema Dkt. Leyna.
Dkt. Leyna amefafanua kuwa Julai mwaka huu wanatarajia kufanya utatifi ili kuona kama watoto akipewa asusa inaweza kuongeza viwango vya damu mwilini na kufikia malengo tarajiwa.
Ameeleza kuwa lengo ni kuhakikisha TFNC inakuwa ni kitivo cha ubunifu wa wajasilimali wadogo wadogo ili kukabiliana na bidhaa zilizopo sokoni ambazo hazina tija kwa lishe ya watoto na vijana.
“Tunatamani tuwe na bidhaa mbalimbali nchini zenye lishe bora na zinapatikana kwa bie nafuu, hivyo mkakati huu unaweza kutufikisha katika malengo husika” amesema Dkt. Leyna.
Mtafiti Mkuu wa Taasisi ya Chukula na Lishe Tanzania Dkt. Anselm Moshi, amesema kuwa mradi wa kutengeneza asusa ni majaribio mdogo ambao yamedumu kwa muda wa mwaka moja, hivyo wanatarajia kufanya mradi mwengine mkubwa kwa ajili ya majaribio.
Dkt. Moshi amesema kuwa mradi huo mkubwa utawafikia watoto wengi kutoka mikoa mbalimbali nchini, huku kieleza kuwa ujio wa wadau hao kutoka china umeleta matumaini ya kufikia malengo na kupata fedha za utekelezaji.
Kwa upande wake Profesa Al Zhao kutoka Chuo Kikuu cha Tsing Hua kutoka nchini China, amesema kuwa bidhaa hiyo ni rafiki kwa watoto katika kutatua changamoto ya ukosefu wa damu katika kuleta majibu sahihi.