Msafara wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi, leo Ijumaa Juni 07, 2024 akiwa njiani kuelekea Tanga, baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku nne Mkoa wa Kilimanjaro kwa kufanya mkutano wa ndani Wilaya ya Same, umesimamishwa na wananchi katika eneo la Hedaru, wakitaka awasalimie.
Akiwa hapo Katibu Mkuu Balozi Nchimbi ameendelea kuwasisitiza Watanzania kuhusu umuhimu wa umoja wa kitaifa kwa kutunza tunu ya amani iliyopo nchini.
Katibu Mkuu wa CCM na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, anaendelea na ziara ya mikoa mitano inayolenga kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2020/2025, kukagua na kuhamasisha uhai wa CCM kuanzia ngazi ya shina, pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia majawabu.