Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) tarehe 04 Juni, 2024 amefanya mazungumzo na Waziri wa Ulinzi wa Ethiopia Mheshimiwa Injinia Ayisa Mohamed Mussa katika Ofisi za Wizara ya Ulinzi nchini Ethiopia.
Mheshimiwa Waziri Tax, yupo nchini Ethiopia akishiriki Mkutano wa kawaida wa 16 wa Kamati Maalum ya Mawaziri wa Ulinzi, Amani na Usalama ulioandaliwa na Umoja wa Afrika (AU).
Katika mazungumzo hayo, Mheshimiwa Dkt. Tax amemshukuru mwenyeji wake kwa mapokezi mazuri, na kusema kuwa Tanzania inajivunia uhusiano mzuri na wa kindugu uliopo baina ya nchi hizo mbili, pia ameelezea utayari wa Tanzania kudumisha ushirikiano huo.
Aidha, Viongozi hao wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika maeneo kadhaa ikiwemo diplomasia ya Ulinzi, katika ngazi ya nchi, Kikanda na Kimataifa.