Jukwaa la Clamate Action Njombe kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya Njombe na halmashauri ya mji Njombe wametoa zawadi kwa shule 22 za sekondari na msingi ambazo zimefanya vizuri katika kutekeleza mpango wa utunzaji wa mazingira nakisha kuhimiza jamii kuendelea kutunza mazingira na matumizi ya niashati safi ili kuinusuru dunia na mabadiriko ya tabia ya nchi.
Akizungumza wakati wa kugawa zawadi hizo Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Njombe amesema lengo ni kuhamasisha vijana ambao ndio taifa la leo na kesho kuwa na uelewa kuhusu umuhimu wa mazingira.
Akisoma Risala kwa Mgeni Rasmi Mjumbe wa Bodi Climate Action Njombe (CAN) kitengo cha Mawasiliano Emilia Msafiri amesema kupitia jukwaa hilo wanatumia mbinu mbalimbali kutoa elimu ikiwemo sanaa ya muziki na vyombo vya habari
Mratibu wa Jukwaa hilo Ibrahim Gabasenyi amesema dunia hufanya maadhimisho hayo kwa lengo la kukabialiana na changamoto ya mabadiliko ya tabia ya nchi na kuwataka watu wanaofanya uharibifu wa mazingira ambao unapelekea athari kama ukame, mafuriko, vimbuga na ongezeko la joto kuacha mara moja.
Baadhi ya wanafunzi waliopata zawadi hizo akiwemo Aida Makweta wamesema kupitia jukwaa la mradi wa Njombe Clamate Action wameanzisha Klabu za Mazingira, wamepanda miti na kutoa elimu kwa jamii kuhusu athari za uharibifu wa mazingira.