Na Mwandishi wetu
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Alhaji Jabir Shakimweri ameipongeza Benki ya Akiba kwa jitihada zake katika kuboresha na kuhifadhi mazingira huku akisisitiza taasisi nyingine kuiga mfano huo .
Pongezi hizo amezitoa leo Juni 5,2024 Dodoma katika hafla ya Uzinduzi wa Viunga vilivyobereshwa vya independence Square na kukabidhi rasmi awamu ya pili ya uboreshaji viwanja hivyo ambapo Benki imekuwa ikijitolea shughuli za kijamii ikiwemo kuhifadhi na kutunza mazingira, ambapo yanaenda samba samba na kaulimbiu ya Siku ya Mazingira Duniani ya mwaka huu, isemayo “Ardhi Yetu, Mustakabali Wetu,”
“Leo ni siku ya Maadhimisho ya Mazingira Duniani Benki ya Akiba katika kusaidia mapambano dhidi ya ukame na majangwa watu wote kila mmoja ana jukumu la kulinda na kuhifadhi mazingira ili kuhakikisha dunia inabaki kuwa mahali salama pa kuishu kwa sasa na vizazi vijavyo” amesema Mkuu wa Wilaya
Naye Meneja wa tawi la Dodoma la Benki ya Akiba, Upendo Makula, amesema Benki ya Akiba imekuwa ikishiriki kikamilifu katika uhifadhi wa mazingira kwa namna mbali mbali kuanzia kupitia huduma zake na ushiriki wa katika shughuli mbali mbali za kijamii pia imepunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya karatasi kwa kuboresha huduma zake za kidijitali, zikiwemo Akiba Mobile, Akiba Wakala, kadi za VISA, taarifa za kielektroniki (E-statement), na huduma za benki Mtandao (Internet Banking)
Sanjari na hayo amesema kuwa huduma hizo si tu kwamba zinapunguza matumizi ya karatasi, bali pia huleta urahisi na uhakika, na kukidhi mahitaji ya soko kwa ufanisi hata hivyo benki hiyo inatoa huduma mbalimbali kama mikopo, akaunti, na bima, zinazowafikia wateja tofauti kuanzia mtu binafsi hadi makampuni makubwa na taasisi za serikali.
Aidha Makula amebainisha kuwa Akiba Commercial Bank inashiriki kikamilifu katika shughuli za jamii za kuhifadhi mazingira kama sehemu ya Sera yake ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).
Mfano halisi ni jitihada zake za muda mrefu za kutunza na kuboresha viwanja vya Independence Square huko Dodoma, jukumu ambalo limekuwa likitekelezwa kwa zaidi ya miaka kumi. Juhudi hizi zinaonyesha nia thabiti ya benki hiyo ya kutunza na kuhifadhi mazingira kwa ajili ya urithi bora wa vizazi vijavyo.