Makamu Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Bara Bw. Tundu Lissu Juni 3, 2024 ameendelea na ziara Mkoa wa Singida ikiwa ni siku ya tatu na kufanya mikutano kwenye Kata ya Ngumanga, Kata ya Ibaga na kumaliza Mkutano wa mwisho Kata ya Nduguti katika Jimbo la Mkalama ambapo amewataka wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga.
Makamu Mwenyekiti ameitaka Serikali kuongeza muda wa zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwani muda wa wiki moja uliotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi hautoshi ukizingatiwa daftari hilo halijafanyiwa maboresho kwa zaidi ya miaka minne sasa.i
Tazama picha za matukio mbalimbali zikionesha matukio mbalimbali ya ziara hiyo ya kukiaanda Chama kuelekea uchaguzi wa Vijiji, Vitongoji na Serikali za mitaa.