Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la dira ya maendeleo 2050 litakalofanyika June 8,2024 katika ukumbi wa Nkurumah chuo kikuu cha Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 4,2024 jijini Dar es salaam Katibu mtendaji ofisi ya Rais,Tume ya mipango Lawrence Mafuru amesema kuwa kongamano hilo linalengo la kukusanya maoni na kutoa elimu kuhusu Tanzania tuitakayo ifikapo 2050.
“Kongamano hili ninkubwa na la kwanza kufanyika hivyo uhamasishaji wa kongamano letu la maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 tunalojukumu la kutoa elimu juu ya Tanzania tuitakayo 2050 ili kuwaandaa vyema wananchi wote kutoa maoni yao ambayo yatachangia kwa asilimia 100 katika kuiandaa Dira 2050”,Amesema Mafuru.
Amesema Tume inatoa wito kwa wananchi wote kila mtu ashiriki katika kutoa maoni yake kwa kutoa majibu ya Je,dira 2050 inamtaka Mtanzania wa aina gani,jamii ya aina gani na nchi ya aina gani ifikapo 2050?
Sambamba na hayo Mafuru amesema kuwa ushiriki wa utoaji wa maoni hayo unaweza kuwa wa aina nyingi ukiwa ni pamoja na kutuma ujumbe mfupi wa simu(SMS),majukwaa ya umma,tafiti,mijadala ya mitandao ya kijamii na mikutano ya kijamii.
Aidha amesisitiza kuwa maoni ya kila mtanzania yanathamni kubwa katika kuandaa dira hiyo hivyo ni vyema kwa kila mtu kushiriki ili kupata Dira itakayokidhi matarajio na mahitaji ya Taifa.
Aidha Mafuru amevitaka vyombo vya habari nchini kuripoti hatua zote za dira kwa kuandaa vipindi vya elimu na kuandaa mahojiano yatakayoendeshwa na tume ili kuongeza uelewa na ushiriki wa umma.
“Vyombo vya habari vinapaswa kuruhusu na kuunda njia kwa wananchi kueleza maoni yao katika vyombo vyenu waweze kuuliza maswali na kutoa maoni juu ya Dira 2050 tunaahidi tume tutafanya kazi kwa karibu na waandishi wa habari pamoja wadau wa maendeleo na mwananchi mmoja mmoja.