Adeladius Makwega-MWANZA.
“Hivi leo tunaadhimisha sherehe ya Mwili na Damu ya Bwana Wetu Yesu Kristo, yeye ni chakula na kinywaji cha Uzima, yeye aliyejiruhusu kujitoa yeye mwenyewe ili atuletee uzima , ili atuletee ukombozi, kwa sadaka yake msalabani na hivi anapoondoka kwetu anabaki kwetu katika maumbi ya mkate na divai, hivyo tunapoadhimisha sherehe hii kubwa ambayo ndiyo kiini cha maadhimisho yote ya kanisa tuna wajibu wa kumshukuru huyu aliyekubali kubaki kati yetu ili tunapokula mwili wake na kunywa damu yake tunaunganika naye na tunapata neema na baraka zake.”
Haya ni maneno ya utangulizi ya misa ya kwanza ya Ekaristi Takatifu -Sherehe ya Mwili na Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo, Juni 2, 2024 Katika Kanisa la Bikira Maria-Malkia wa Wamisionari , Parokia ya Malya, Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza iliyoongozwa na Padri Samson Emmanuel Masanja.
“Mimi ndimi chakula chenye uzima; mtu akila chakula hiki ataishi, asema Bwana.”
Hivyo ndivyo alivyoanza mahubiri yake Padri Masanja huku akibainisha sherehe ya Ekaristi ilianza kusherekewa mwaka 1254 na Baba Makatifu Urban wa IV ambayo ilikuwa ikipambwa kwa shangwe na maandamano makubwa.
Padri Masanja akiendelea kuhubiri aliuliza swali hili.
“Je Ekaristi Takatifu ni nini?”
Aijibu
“Ekaristi Takatifu tunatazama uwepo wa Yesu Kristo katika maumbo ya mkate na divai, sadaka hii ni zaidi ya sadaka za kujinja ya wanyama na kuteketeza, hapa amejitoa Kristo yeye mwenyewe.”
Padri Masanja alisisitza kuwa hapa tunapompokea Yesu wa Ekaristi Takatifu kila ampokeaye ana wajibu wa kuwa kweli safi wa Roho maana anayempokea ni Yesu Mwenyewe,
“Jamani tunapompokea lazima tuwe tumejiandaa.”
0717649257