Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Comrade Daudi Yassin leo Juni 2, 2024 ameongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Iringa.
Kikao hicho ambacho pia kilihudhuriwa na Comrade Salim Abri Asas, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Mkoa wa Iringa na Comrade Richard Kasesela Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Bara) kilijadili masuala mbalimbali yenye lengo kuendelea kuimarisha chama hicho.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho, Comrade Yassin amesisitiza suala la umoja na mshikamano kama njia ya kuendelea kujiimarisha.
Amesema hata kama zitafanyika bwembwe za aina gani ikiwa CCM haitashinda chaguzi zote ni kazi bure.
Mwenyekiti Yassin ameeleza kuwa heshima ya CCM ni kushinda uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu hapo mwakani kwa sababu Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan inatekeleza Ilani ya CCM kwa kiwango kikubwa
Pia wabunge akiwemo David Kihenzile (Mufindi Kusini), Justine Nyamoga (Kilolo), Jackson Kiswaga(Kalenga), Ritha Kabati (Viti Maalum) na Nancy Nyalusi (Viti Maalum) walipata nafasi ya kutoa salamu kwa niaba ya wananchi wanao wawakilisha.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Peter Serukamba ametaja mambo anayo simamamia kuwa ni kumalizia miradi, ukusanyaji wa mapato na kushughulikia kero za wananchi.
Wakuu wa Wilaya za Mufindi, Kilolo na Iringa Mjini waliahidi kuendelea kusimamia utekelezaji wa Miradi ya maendeleo kwenye wilaya zao.
Kwa pamoja, wenyeviti wa CCM wa Wilaya zote za Mkoa wa Iringa wameahidi kuchapa kazi wakimuhakikishia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa ushindi wa kishindo kwenye chaguzi zijazo.