Na Farida Mangube
Chuo kikuu Mzumbe kimefanikiwa kupata wahadhiri 12 wenye shahada ya uzamivu waliotokana na mradi wa 4site program uliofadhiliwa na nchi ya Ubeligiji kupitia vyuo vikuu vine kutoka nchini humo huku vijiji 15 vya wilaya ya Mvomero mkoani morogoro vikinufaika na mradi huo uliodumu kwa miaka 11 ukisaidia katisha masuala mbalimbal kwa kuwajengea uwezo viongozi wa serikali za mitaa juu ya utawala bor,pamoja na upatikanaji wa maji safi na salama katika vijiji hivyo.
Hayo yameelezwa na makamo mkuu wa Chuo kikuu cha Mzumbe Profesa Wiliam Mwigoha wakati wa hafla ya ufungaji wa mradi wa 4SITE PROGRAMM uliodumu kwa muda wa miaka kumi na mmoja na kuhudhuriwa na Balozi wa Ubeligiji hapa nchini Peter Rogbret, viongozi wa Serikali ya Wila ya Mvomero,wadau wengine pamoja na wanafunzi wa chuo hicho.
Katika hotuba yake makamo mkuu wa chuo kikuu Mzumbe Profesa Mwigoha amesema kuwa mradi huo ulikuwa na manufaa makubwa kwa chuo na jamii ya wakazi wa wilaya ya Mvomero na kwamba Mzumbe itaendelea kuyafanyia kazi na kuendeleza yale yote yaliyotokana na mradi huo.
Aidha amesema kuwa mradi huo umeweza kuwajengea uwezo katika upande wa Tehama kwa ajili ya utengenezaji wa mataala na kubadilisha njia za ufundishaji chuoni hapo pamoja na kupata wataalamu katika upande wa ubunifu ambao wote wameingia katika mfumo wa ajira na watakisaidia chuo kwa kiwango kikubwa.
“Mradi huu umetusaidia kwa kiasi kikubwa na tunashukuru sana vyuo vikuu vya ubeligiji kwa ufadhili wake na ushirikiano huu utaendelea kuwepo ili kuwezesha mambo mengi zaidi kufanyika katika chuo kikuu Mzumbe na jamii ya watu wa wilaya ya Mvomerp”
Kwa upande wake mkuu wa Ewilaya ya Mvomero Judith Nguli ameshukuru nchi ya Ubeligiji kwa kufadhili mradi huo kwani jamii ya wakazi wa wilaya ya mvomero wamenufaika kwa kiasi kikubwa huku akiomba ufadhili uendelee kwa kuja na mradi mwingine hasa utakao saidia katika kutatua tatizo la mabadiliko ya mabianchi.
“Tunashukuru sana kwa kutusaidia katika masuala ya maji na kuwajengea uwezo viongozi wetu wa serikali za vijiji na Tunazidi kuomba sana kupitia chuo kikuu Mzumbe nchi ya Ubeligiji itutazame pia kwa jicho la kipekee kwenye tatizo la mabadiliko ya tabianchi ambalo linazidi kuathiri wilaya yetu kila kukicha.
Kwa upande wake balozi wa Ubeligiji hapa nchini Peter Rogbret ameshukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mzuri uliopo baina ya nchi hizo huku akieleza kuwa Ubeligiji kupitia vyuo hivyo itaendelea kushirikiana na chuo kikuu Mzumbe ili kujenga jamii zilizobora zaidi.