NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
BANDA la Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), limekuwa kivutio kwa wakazi mbalimbali wa Jiji la Mwanza baada ya kujitokeza kupata elimu ya masuala mbalimbali na bima ikiwemo ya kilimo.
Akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda hilo la TIRA leo, Ofisa Ubora na Mtaalam wa Bima (QRMO), Isango Halfan amesema bima ya kilimo inalenga kumfidia mkulima anapopata hasara iliyosababishwa na athari za uzalishaji kama ukame, mafuriko,wadudu au magonjwa ya mazao yasiyotibika.
Aliyataja mazao yanayolindwa kwa kukatiwa bima ni kahawa, pamba, mahindi, korosho,mpunga,shairi,alizeti,
“Bima inacholinda dhidi ya mazao hayo ni ukame,mafuriko,magonjwa na wadudu wanaotibika na wasiotibika,vimbuga na mvua ya mawe,”amesema Halfan.
Amesema katika maenesho ya mwaka huu wanatoa elimu ya bima kwa wakulima na wafugaji pia kufahamu changamoto zao ili kuwahudumia kwa ubora zaidi na hadi sasa wamewahudumia watu zaidi ya hamsini.
Mtaalamu huyo wa bima amesema kinachohitajika kutoka kwa mkulima ni fomu ya maombi iliyojazwa na kusainiwa,gharama za uzalishaji kwa ekari,makadirio ya gharama ya bei kwa kilo,taarifa za uzalishaji za historia ya mkulima.
Makadirio ya fidia huzingatia upungufu wa uzalishaji kwa kiwango kilichofanyiwa tathmini baada ya majanga husika kutokea ambapo malipo ama fidia hufanyika mwshoni mwa msimu na kufafanua gharama ya bima huanzia asilimia tatu hadi sita ya gharama za uzalishaji.