………………….
Na Sixmund Begashe, Bungeni Dodoma
Wizara ya Maliasili na Utalii, inaendelea na jitihada za kuifungua zaidi kanda ya Kusini kiutalii wa Malikale ili kuvutia watalii wengi zaidi kutembelea vivutio vilivyopo Kusini mwa Tanzania pamoja na kuwainua wananchi kiuchumi.
Hayo yamesemwa leo Bungeni Dodoma na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki alipokuwa akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025
Mhe. Kairuki katika kuhakikisha kuwa maeneo ya malikale yanaendelea kukidhi vigezo vya kimataifa na kuvutia watalii, Wizara imefanikiwa kupandisha hadhi Eneo la Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara, lenye Hadhi ya Urithi wa Dunia kuwa miongoni mwa maeneo yenye mahusiano ya kisayansi kati ya binadamu na mazingira (Man and Biosphere Reserve).
“Hadhi hiyo imetolewa na UNESCO mwezi Julai, 2023 na hivyo kuongeza idadi ya maeneo yenye sifa hiyo nchini kutoka 5 hadi 6” Waziri Kairuki
Aidha, Mhe. Kairuki ameongeza kuwa, mafanikio hayo yamechochea shughuli za utalii wa malikale kwa kuongeza idadi ya watalii wa Kimataifa katika eneo la Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara hususan kupitia utalii wa meli