Mwamvua Mwinyi, Rufiji
Mei 31
Mnada wa zao la kibiashara la Ufuta, unatarajia kufunguliwa Juni 5 mwaka huu , Wilayani Kibiti mkoani Pwani.
Hayo yamebainika katika mkutano wa wadau wa Ufuta mkoani humo, mkutano ambao umeongozwa na Mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge .
Aidha Kunenge ameeleza kwa mwaka 2023/24 uzalishaji ulikuwa Tan 15,000 na kuingizia wakulima kiasi cha shilingi Bilioni 57.8.
Amesema, kwa mwaka huu wataendelea kutumia mfumo wa Stakabadhi ghalani na wanategemea kuwa na uzalishaji wa zaidi ya Tan 20,000.
Kunenge amewataka wakulima kusimamia ubora wa ufuta wao kwa kutochanganya na mchanga au pumba.
Vilevile amekitaka Chama Kikuu cha Ushirika CORECU kuangalia uwezekano wa kuanzisha kiwanda cha kuchakata ufuta ili kuongeza thamani.