Mhe. Allu Nzowa Hakimu Mkazi mfawidhi Mkuu wa Mahakama ya hakimu mkazi Singida akifungua mafunzo ya maadili kwa waheshimiwa mahakimu wa mkoa wa Singida yaliyolenga umuhimu wa hati ya Ahadi ya Uadilifu. Mafunzo yalifanyika tarehe 31 Mei, 2024 katika ukumbi wa Jalim mkoani Singida na kuandaliwa na Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kanda ya Kati.
Bw. Joshua Mwambande Afisa Maadili kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma akiwasilisha mada kuhusu tamko la zawadi kwa waheshimiwa mahakimu wa mkoani Singida katika mafunzo yaliyofanyika tarehe 31 Mei, 2024 katika ukumbi wa Jalim Singida.
Baadhi ya waheshimiwa mahakimu wa mkoa wa Singida wakifuatilia mada mbalimbali za maadili kwa viongozi zinazowasilishwa na maafisa kutoka Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kanda ya kati Dodoma, mafunzo hayo yalifanyika tarehe 31 Mei, 2024 katika ukumbi wa Jalim mkoani Singida.