Na Fredy Mgunda, Nachingwea
MADAKTARI bingwa wa Dkt Samia Suluhu Hassan kuwatibu zaidi ya wagonjwa 600 wenye magonjwa mbalimbali katika wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi kwa siku 5
Akizungumza wakati uzinduzi wa zoezi hilo, mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo amewataka wananchi kutumia vizuri nafasi hiyo kupata huduma za kibingwa.
Moyo aliwaomba wananchi kuwafikishia taarifa wananchi wengine ambao wanahitaji msaada wa huduma za matibabu ya kibingwa katika wilaya ya Nachingwea na madaktari bingwa wa DKT Samia watakaa kwa siku tano Nachingwea.
Jumla ya Madaktari bingwa sita wamewasili Wilaya ya Nachingwea na Huduma zitakazotolewa ni pamoja na huduma za upasuaji, ganzi na usingizi, matibabu ya ngozi, huduma za Afya kwa watoto, magonjwa ya ndani na magonjwa ya wanawake na uzazi. Huduma hizo zitatolewa na Madaktari hao kwa muda wa siku tano.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Mhandisi Chionda Kawawa alimshukuru Rais Dr Samia suluhu Hassan kwa kuwapeleka madaktari bingwa katika Halmashauri hiyo.
Mhandisi Kawawa alisema wananchi wanapaswa kuitumia vizuri fursa ya uwepo wa madaktari bingwa katika Halmashauri ya Nachingwea.