Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi wakipata maelezo juu ya kifaa cha ECG Mashine kinavyofanya kazi walipotembelea banda la MUHAS katika Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Ujuzi, Elimu na Ubunifu yanayofanyika Jijini Tanga
Baadhi ya Wanafunzi wa sekondari wakipata maelezo ya mashine ya AHG katika Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Ujuzi, Elimu na Ubunifu yanayofanyika Jijini Tanga
Baadhi ya Wanafunzi wa sekondari wakipata maelezo ya program tumizi ( application) ya Afya AI jinsi inayofanya kazi katika Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Ujuzi, Elimu na Ubunifu yanayofanyika Jijini Tanga
Wanafunzi wa sekondari wakiangalia bidhaa zinavyozalishwa chuoni MUHAS katika skuli ya famasia
Wanafunzi wakipata melezo ya ubunifu wa Mlo Hub katika Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu Jijini, Tanga
Wanafunzi wakipata maelezo ya program zinazotolewa chuoni MUHAS wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu, Jijini Tanga
Mbunifu kutoka MUHAS akielezea bunifu yake wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa Ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu, Jijini Tanga.
Wabunifu kutoka MUHAS wakiwa kwenye picha ya Pamoja katika Maadhimisho ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu, Jijini Tanga.
………………
Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili ( MUHAS) kinashiriki Maadhimisho ya Wiki ya Taifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika katika viwanja vya shule ya sekondari Popatlal jijini Tanga.
Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili ( MUHAS ) kimeendelea kuwa kivutio kwa wananchi wanaotembelea banda hilo kwa kuonesha bunifu mbalimbali zilizobuniwa na wahadhiri na wanafunzi kutoka MUHAS.
Kati ya Bunifu hizo ni Programu tumizi(Application) inayoitwa AFYA AI ni bunifu iliyobuniwa na mwanafunzi kutoka MUHAS,, Ni App ya simu janja inayotumia teknolojia ya akili mmende ( Artificial Intelligence) kumuwezesha mtumiaji wake kutambua uwezekanao wa kupata magonjwa ya presha na kisukari kisha kupendekeza hatua za kuchukua ili kuepeuka magonjwa hayo na pia inamsaidia mtumiaji kujifanyia tathmini ili kujua kuna hatari ya ukubwa kiasi gani ya kupata magonjwa ya presha na kisukari.
Vile vile ubunifu wa mfumo wa Mama Care mfumo unaowawezesha watoa wa huduma za afya nchini wenye elngo la kutatua changamoto za uzazi kwa kutumia teknolojia ambayo inahakikisha wanawake wajawazito wanajifungua salama na wanapata ufatiliaji mzuri wakati wa leba.
Pia kuna program tumizi (application) inayoitwa Pona Health Ni app inayoshughulika masuala mbalimbali ya kiafya ya uzazi , shinikizo la damu, kisukari afya ya akili, na pia ni app inayotoa elimu kuhusu masuala ya ustawi wa jamii.
Bunifu nyingine ni kifaa kinachotunia teknolojia ya kisasa ya utambuzi wa magonjwa ya moyo – ECG Stereo, MLO HUB ambalo ni jukwaa la kidigitali linalowezesha wauzaji kuthibiti biashara zao na kuboresha afya ya walaji kwa kutoa ushauri wa lishe bora, Maternal Point of Care ni mfumo wa kidigitali uliokusudiwa kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa kuwawezesha wajawazito na watoa huduma katika mchakato wa huduma za afya ya uzazi, na bunifu nyingine pia ni AHG Mashine ambayo ni kifaa cha kuzalisha joto kiotomatiki, na bunifu ya Akili Plus ni app inayotoa ushauri wa kitaalamu ili kuimarisha ustawi wao wa kiakili.
Katika maadhimisho haya wananchi wanapata fursa ya kufahamu program mbalimbali zinazotolewa chuoni Pamoja na bidhaa zinazozalishwa chuoni hapo.