Mwanafunzi Mbunifu- Kutoka MUHAS, Ethan Magubika akielezea bunifu yake ya Pona Health kwa mtaalamu kutoka Roboteck Labs alipotembelea banda la MUHAS wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Ujuzi , Elimu na Ubunifu, Jijini Tanga
Bw. Abdulwahab Issa kutoka Roboteck Lab akitoa maelezo wakati alipotembelea banda la MUHAS
Mbunifu kutoka MUHAS akielezea bunifu yake ya Afya AI wakati kwa mtaalamu kutoka Roboteck Lab alipotembelea banda la MUHAS
Wataalamu kutoka Riboteck Lab wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kuzungumza na wabunifu.
………………….
Kampuni ya Roboteck Lab yakutana na wabunifu kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili( MUHAS) kwa ajili ya kuwapa elimu juu ya kuwa na bunifu zinazozingatia kiwango vya kimataifa, maadili ya nchi na usalama kwa mtumiaji hasa kwa bunifu zinazotumia proramu tumizi ( Applications)
Akizungumza kwenye mkutano huo, Bw. Abdulwahab Issa kutoka Kampuni ya Roboteck Labs aliwasisitiza wabunifu kutoka MUHAS kushirikiana na wataalamu wa masuala ya program tumizi ili kuwasaidia kuwa na bunifu zenye viwango na zinazofuata taratibu za nchi.
“Kampuni yetu inatoa msaada wa kitaaluma kwa anayehitaji tupo tayari kushirikiana katika kuhakikisha bunifu zenu zinafata viwango vya kimataifa”’, Amesema Bw. Issa.
Naye Mratibu wa Ubunifu kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili ( MUHAS), Dkt. Nelson Masota amesema Kurugenzi ya Tafiti, Machapisho na Ubufunifu wataandaa mafunzo maalumu kwa ajili ya wabunifu kutoka MUHAS na pia kuingia mkataba wa makubaliano na kampuni hii kuona jinsi gani watashirikiana katika kuboresha kazi za wabunifu kutoka MUHAS.
Mkutano huu umefanyika katika Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayoendelea jijini Tanga katika shule ya sekondari Popatlal na vile vile katika mkutano huu wabunifu walipata fursa ya kuuliza maswali kwa wataalamu kutoka Kampuni ya Roboteck Lab.