Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba amewataka viongozi wa ushirika wa Wachimbaji wadogo wa Madini ya dhahabu wa Mgusu,kumaliza migogoro ambayo himo Ndani ya ushirika huo.
Wito huo ameutoa mapema Leo wakati akizungumza kwenye Mkutano maalum wa ushirika wa Mgusu ambao umefanyika kwenye Kata ya Mgusu.
Amesema jambo la msingi ambalo viongozi wa ushirika huo wanatakiwa kuzingatia na kutatua ni kuondoa migogoro yao Pamoja na kuvumiliana kwa Kila jambo ambalo linaonekana lipo tofauti na matakwa yao.
“Watu mia nane amuwezi kuwa na mawazo ya kufanana niwaombe tu Ndugu zangu tusiwe Watu wa kukumbatia migogoro badala yake tuwe watatuzi itatusaidia kwenda mbele zaidi kimaendeleo”Hashim Komba Mkuu wa Wilaya ya Geita.
Aidha Komba amesisitiza Mambo ya Msingi ambayo wanaushirika wanatakiwa kupata ni Elimu ya kutosha Juu ya uwekezaji unaenda kufanyika ndani wanaushirika wa Mgusu.
“Na kwasababu Moja ya Changamoto ulikuwa ni Mkataba ni vyema mkawasomea wanaushirika neno kwa neno hili wao wajue kile ambacho mnakwenda kuweza kwa muwekezaji”Hashim Komba Mkuu wa Wilaya ya Geita.