Askari Polisi nchini wamehimizwa kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuzingatia weledi na ufanisi mahala pa kazi na kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi, kuepuka lugha chafu na manyanyaso kwa wanaowahudumia ili kuendana na falsafa ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter SeRukamba wakati wa hafla ya uvishaji wa Nishani kwa maafisa, wakaguzi na askari wav yeo mbalimbali zoezi ambalo limefanywa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura kwa niaba ya Mhe. Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Naye Mnec taifa Bwana Salim Abri amesema kuwa, kwa sasa matukio ya uhalifu yamepungua nchini hasa uhalifu wa ujambazi na kutumia silaha za moto kutokana na weledi na uchapakazi wa askari wa Jeshi la Polisi katika kushughulikia makosa ya uhalifu nchini.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura amesema kuwa, kitendo cha Mhe. Rais kutunuku nishani maafisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali kimeongeza tija kwa askari Polisi na kwamba bado mhe. Rais ameendelea kuliboresha Jeshi la Polisi kwa kuliongezea vitendea kazi mbalimbali ili kuwa na Jeshi bora na la kisasa`linalotoa huduma sahihi kwa wananchi ambapo Jeshi limeapa kuwalinda wao na mali zao.