Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameshiriki zoezi la upandaji wa miti aina ya Mdodoma katika eneo la Zahanati ya Kapanga, iliyopo Kijiji cha Kapanga, Kata ya Katuma, Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi leo tarehe 28 Juni, 2024.
Dkt. Jafo ametembelea mkoa huo kufuatilia utekelezaji wa miradi ya Kaboni na faida zilizopatikana kupitia biashara ya kaboni ambayo imewezesha Halmashauri ya Tanganyika kufanya maendeleo makubwa ikiwemo ujenzi wa Zahanati ya Kapanga, vyoo, kichomeo taka pamoja na nyumba mbili za watumishi wa Zahanati hiyo.
Ziara hiyo imefanyika wakati wa kuelekea maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani tarehe 5 Juni, 2024 ambapo atazindua shughuli zinazotekelezwa na mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bioanui Tanzania (SLR) unaotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.