Wahandisi wakipata huduma katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa Mkutano wa 30 wa wahandisi washauri Afrika (FIDIC Africa) unaofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere International Convention Center (JNICC) uliopo jijini Dar es Salaam.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Faizat Ndosa akimpima sukari kwenye damu mhandisi aliyetembelea banda la JKCI wakati wa mkutano wa 30 wa wahandisi washauri Afrika (FIDIC Africa) unaofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere International Convention Center (JNICC) uliopo jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa huduma za afya za mtandao kutoka kampuni ya Cloudscript inayofanya kazi na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Beatrice Mmari akiwafundisha wahandisi namna ya kutumia huduma ya afya mtandao kupitia mfumo wa Cloudscript walipotembelea banda la JKCI wakati wa mkutano wa 30 wa wahandisi washauri Afrika (FIDIC Africa) unaofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere International Convention Center (JNICC) uliopo jijini Dar es Salaam. Picha na: JKCI
…….
Na: Mwandishi Maalumu – Dar es Salaam
28/05/2024 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inatoa huduma za uchunguzi wa magonjwa ya moyo na ushauri wa lishe bora kwa wahandisi kutoka nchi za Afrika walioudhuria mkutano wa 30 wa wahandisi washauri Afrika (FIDIC Africa).
Huduma hiyo inatolewa kwa siku mbili katika viwanja vya ukumbi wa kimataifa wa mwalimu Julius Nyerere International Convention Center (JNICC) vilivyopo jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia huduma hiyo daktari kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Samweli George alisema JKCI imeona umuhimu wa kuwasogezea wahandisi huduma za uchunguzi wa magonjwa ya moyo karibu kuwapa nafasi ya kuchunguza afya zao.
“Waandisi muda mwingi wanakuwa katika maeneo yao ya kazi (site) na kukosa nafasi ya kufika Hosptitali kwaajili ya kuchunguza afya hivyo kupitia mkutano huu tunawapa nafasi ya kupima afya lakini pia tunawapa elimu ya namna ya kujikinga na magonjwa ya moyo”, alisema Samweli
Katika kutoa elimu ya mfumo bora wa maisha Dkt. Samweli aliwataka wahandishi kuwa na tabia ya kuchunguza afya zao mara kwa mara na kuijua miili yao kwani magonjwa ya moyo wakati mwingine humtokea mtu bila ya kuonyesha dalili.
Kwa upande wake Mhandisi kutoka Tanroad Magdalena Evance aliwashukuru wataalamu wa afya kutoka JKCI kwa kumfanyia uchunguzi wa afya kwani hajawahi kuchunguza afya yake kama hana changamoto yoyote ya ugonjwa.
“Leo nimejifunza kitu kikubwa sana katika maisha yangu, natakiwa kuchunguza afya yangu kila ninapopata nafasi na nisisubiri hadi niumwe kwasababu tumeambiwa magonjwa yasiyoambukiza wakati mwingine hayana dalili”, alisema Magdalena
Magdalena alisema baada ya kupima amepata ushauri wa namna ya kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza elimu ambayo ataizingatia kwani kinga ni bora kuliko tiba.