Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson katikati akipewa maelezo ya namna karakana inayotembea inavyofanya kazi na fundi wa karakana hiyo Mustafa Abdul Malambo wakati alipotembelea kujionea namna karakana hiyo inavyofanya kazi leo Tarehe 27 Mei, 2024 katika Maonesho ya Sekta ya Ujenzi yanayofanyika katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma. Kulia kwake ni Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa na Katibu Mkuu Ujenzi Mh. Balozi Aisha Amour.