Serikali ya Comoro imeahidi kuunga mkono ugombea wa Mhe Dkt Faustine Ndugulile katika nafasi ya Ukurugenzi wa Kanda wa Shirika la Afya Duniani (WHO).Hayo yameelezwa na Mheshimiwa Dhoihir Dhoulkamal,Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro baada ya kuombwa rasmi na Balozi wa Tanzania Nchini humo aliefika kujitambulisha na kuwasilisha nakala ya hati zake za Utambulisho.
Awali akijitambulisha Balozi Yakubu aliipongeza Serikali ya Umoja wa Visiwa vya Comoro kwa sherehe nzuri za Uapisho wa Rais Azali Assoumani ambazo zilihudhuriwa na wakuu wa nchi mbali mbali ambayo ni ishara ya mtazamo mzuri wa mataifa ya nje kwa nchi hiyo.
Katija mazungumzo yao,Balozi Yakubu alifikisha pia salamu za Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan za azma yake ya kuona mahusiano ya Tanzania na Comoro yanakuwa juu zaidi na ushirikiano unaongezeka katika nyanja nyingi zaidi.
Balozi Yakubu aliwasilisha mwaliko maalum wa kuomba ushiriki wa Comoro katika maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Saba Saba) ambao ulikubaliwa.