Mashindano ya vitivo Chuo Kikuu Mzumbe Kwa mwaka huu 2024 yamehitimishwa Mei 26, yakihusisha michezo mbalimbali na washindi kuondoka na zawadi ya Kombe, mipira na jezi.
kila mwaka Mzumbe imekuwa ikiandaa mashindano hayo Kwa lengo la kukuza taaluma, vipaji, na mshikamano miongoni mwa wanafunzi.
Akifunga mashindano hayo Kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha, Amidi wa wanafunzi Bw. Alphonce Kauky amewapongeza waandaaji wa mashindano na washiriki Kwa kuonesha ushindani ukubwa.
Katika mashindano hayo washindi walipata zawadi mbalimbali pamoja na Fedha taslimu, kwenye mpira wa miguu Shule ya Sheria aliibuka kidedea Kwa kuichapa goli moja Kwa sifuri kitivo Cha Sayansi na Teknolojia.