VIJANA wa chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa wametakiwa kujikita katika siasa na uchumi kwa sababu bila kuwa na uchumi imara huwezi kufanya siasa unaitaka.
Akizungumza wakati Mafunzo kwa baraza la vijana Wilaya ya Iringa Mjini,Katibu wa siasa na uenezi Mkoa wa Iringa Joseph Ryata alisema kuwa serikali ya awamu ya sita imekuwa ikitoa fursa nyingi za kiuchumi kwa vijana hivyo ni jukumu la vijana kuchangia fursa hizo.
Ryata alisema kuwa Rais Dr Samia suluhu Hassan anatoa mikopo ya asilimia 10 kwenye halmashauri zote nchi nzima ikiwepo Iringa hivyo kimoja ya fursa huku akiitaja fursa ya utalii ambayo kwa sasa mkoa wa Iringa imeshika kasi.
Alisema kuwa katika mkoa wa Iringa vijana wanafursa ya kufanya kilimo cha umwagiliaji kwa kuwa Rais Dr Samia suluhu Hassan amewekeza Mradi wa umwagiliaji wa billion 57 Pawaga huku wakiendelea kuwatafutia masoko ya nje kwa wakulima wa mazao mbalimbali wa mkoa wa Iringa.
Ryata alimalizia kwa kuwataka vijana kujikita kwenye siasa za kimaendeleo ambazo zinatija kwa taifa na sio siasa za kupoteza amani iliyopo Tanzania.