Wanafunzi wa chuo cha Abdul -rahman Alsumait wakifanya mchezo wa kushindana Kula matikikiti katika bonanza lililowashirikisha wanafunzi na wafanyakazi wa chuo hicho ambapo halima ambae ni mfanyakazi aliibuka ushindi wa kwanza.
NO.09:-Matron wa wanafunzi wakike katika Chuo cha Abdul Rahman Al-Sumait Hawa Said Abdalla akimkabidhi kombe Mwakilishi wa Timu ya wanafunzi baada ya kuibuka ushindi WA bao 22-14 katika mechi ya valleyball iliyochezwa Kati tao na Timu ya wafanyakazi huko Chikwani Zanzibar.
……………………
Na Fauzia Mussa maelezo. 26.05.2024.
Wanafunzi wa kike wametakiwa kushiriki katika michezo mbalimbali hata wanapomaliza masomo ili kulinda vipakji vyao.
Hayo yameelezwa na Mlezi wa wanafunzi wa kike katika Chuo Kikuu cha Abdul Rahman Al-Sumait Hawa Said Abdalla mara baada ya kukamalizika bonaza la michezo, lilioshirikisha timu ya wanafunzi na waalimu wa Chuo hicho huko chukwani Wilaya ya magharibi B.
Amesema ushiriki wa Wanawake katika michezo ni mdogo hasa wanapokuwa majumbani kutokana majukumu ya familia ikiwemo kazi za ndani.
Hivyo amewaomba wazazi kugawa majuku sawa ya nyumbani kati ya Wanawake na Wanaume ili kutoa fursa ya Wanawake kushiriki katika michezo.
“michezo inasaidia kujenga na kuimarisha Afya na akili na kuwataka Wanafunzi kuiendeleza michezo hata baada ya kuondoka skuli na vyuoni.” amesema Matron
Aidha amezishauri Taasisi za Serikali na binafsi kuwashirikisha wanawake katika michezo ili kupata nafasi ya kuendeleza vipaji walivyokuwa navyo wakati walipokuwa skuli na kuweza kuwaletea maendeleo.
Mbali na hayo amewaomba Wanawake wanaoshiriki michezo kuvaa nguo za stara na heshima ili kulinda silka, desturi na tamaduni za mzanzibari na kuwa mfano nzuri kwa wengine watakaojiunga katika michezo.
Bi Safia Ali Hassan ni mmoja kati ya wanakamati ya michezo katika Chuo Kikuu cha Abdul Rahman Al-Sumait amewaomba wadau wa michezo kuendelea kuhamasisha na kutoa elimu kwa jamii ili kuongeza ushiriki wa wanawake katika michezo.
” Sisi wanawake tunaoshiriki michezo tuwe mabalozi wazuri kwa wenzetu katika kuelimisha wanawake kushiriki michezo ili kutoa hamasa kwa wanawake wengine kupenda michezo.” Alisema Mwanakamati huyo.
Nao Baadhi ya Wanafunzi walioshiriki katika bonaza hilo akiwemo Anita Melka na Fatuma Madimbwala wamewashauri wanafunzi wenzao na wanawake kwa ujumla kushiriki michezo kwani kunajenga umoja, upendo, mashirikiano na kujipatia ajira.
“Kwa mfano huyu matron wetu anafika mbali kwa kuwapeleka wanafunzi kushiriki michezo, analipwa kupitia michezo, sio kila mtu anaweza atatoboa kupitia elimu ya darasani, tunaona wapo wengi tu wanaofanikiwa kupitia michezo mbalimbali.” walisema wanafunzi hao.
Hata hivyo wamewashauri wazazi kuwapa nafasi Watoto wao wa kike kushiriki michezo kama wanavyowapa watoto wa kiume kwani michezo ni haki ya kila mtu.