Adeladius Makwega-MWANZA
“Enendeni duniani kote, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wangu, mkiwabatiza kwa Jina La Baba, Kwa Jina la Mwana na Kwa Jina Roho Mtakatifu-Amina.”
Haya ni maneno ya utangulizi ya mahubiri Jumapili ya Utatu Mtakatifu katika Misa ya Jumapili ya Mei 26, 2024 iliyoongozwa na Padri Samsoni Masanja, ikiwa ni mojawapo ya mahubiri mafupi kuliko yote ambayo Mwandishi wa Ripoti hii ameyashudia kwa kipindi cha mwaka 2023 na 2024 na huku yakieleweka vizuri katika misa zilizoongozwa na Padri Masanja ndani ya Kanisa la Bikira Maria-Malkia wa Wamisionari, Parokia ya Malya iiyopo katika Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza nchini Tanzania.
Padri Masanja akitilia mkazo juu ya Utatu Mtakatifu alisema maneno haya;
“Hii ni sherehe inayomuambatanisha Mwenyeenzi Mungu katika nafasi tatu; Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu.Tunapoadhimisha sherehe hii tumuaadhimisha Mungu wa Uumbaji, Mungu wa Ukombozi na Mungu wa Utakatifusaji wa Mungu. Katika nafsi hizo tatu mambo hayo makuu yanatendeka.”
Padri Masanja aliongeza kuwa sherehe ya Utatu Mtakatifu inaadhimisha fumbo zito lakini itoshe kusema Utatu Mtakatifu ni Mungu mmoja katika nafsi tatu. Ushahidi wake unaonekana wazi wazi katika mambo haya;
“Kwanza wakati Yesu anabatizwa; Sauti kutoka Mbinguni ilimtambulisha, ‘Huyu Ndiye Mwanangu Mpendwa Niyependezwa naye Msikilizeni.’ Tunaa mbiwa mara baada ya huo ubatizo alishukiwa na Roho Mtakatifu kwa mfano wa njiwa mabegani mwake huo ni uthibitisho wa pili. Hapa tunasikia Sauti ya Mungu Baba ikisema, tunaona Mungu Mwana akibatizwa na tunamuona Mungu Roho Mtakatifu akimshukia huyo anayebatizwa. Tukio la pili ni maagizo ya Yesu Mwenyewe anawaambia wanafunzi wake enendeni ulimwenguni kote mkawabatize watu kwa Jina la Baba,na la Mwana na Roho Mtakatifu.”
Padri Masanja alimalizia mahubiri yake akisema kuwa sherehe hii jukumu lake ni kutukomaza katika imani yetu.
Mwanakwetu Upo? Kumbuka,
“Utatu Mtakatifu Utukomaze Katika Imani Yetu.”