Na Prisca Libaga Arusha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Arusha imetoa elimu juu ya madhara ya tatizo la dawa za kulevya na rushwa kwa wazee 35 kutoka Kata 25 za Jiji la Arusha katika Ukumbi wa Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini. Mgeni rasmi wa semina hii maalum alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Mhe. Felician Mtahengerwa.
Aidha, kundi la wazee ni kundi muhimu sana sababu ya hekima na busara walizonazo katika jamii. Hivyo, elimu waliyoipata wazee itakuwa chachu ya wazee hao kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya nchini.