Na Sophia Kingimali.
Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki January Makamba amesema dhamira ya Afrika ni kunyamazisha bunduki ifikikapo 2030 na bara kuwa na usalama na amani.
Hayo ameyasema leo May 25,2024 jijini Dar es salaam kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza la amani na usalama la umoja wa Afrika (PSC-AU)
Amesema kongamano la amani na usalama Afrika limelenga zaidi kujadili changamoto za kiusalama na kuonesha dhamira ya kuimarisha amani na usalama katika bara hilo.
” Tumethibitisha dhamira yetu ya dhati ya kuimaraisha amani,usalama na ustawi wa Afrika kama ilivyo katika nchi yetu ambayo tumekuwa kitovu cha usalama na amani katika bara letu”,Amesema.
Aidha Makamba amesema Tanzania ipo tayari kuendelea kuunga mkono jitihada za kuhakikisha Afrika iliyoungana na kuwa na mafanikio na pia kuwa na dhamira ya dhati kutokomeza vita kwa vizazi vijavyo.
Ameongeza kuwa uendelezaji wa Afrika huru,umoja na yenye amani na ustawi bado uwezo wa baraza ni mdogo hivyo Tanzania itaendelea kusaidia kwa kiasi kikubwa uwepo wa usalama na amani katika bara zima la Afrika.