Wataalamu wa mifumo ya TEHAMA wa Wizara ya Maji wamepongezwa kwa kuanza kazi ya kuitengeneza mifumo yote katika wizara kusomana.
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Kundo Mathew (Mb) ametoa pongezi hiyo baada ya kutembelea timu inayofanya kazi hiyo na kuongea nayo.
“Kazi hii itaondoa utitiri wa mifumo na kuondoa changamoto ya utekelezji wa majukumu” Mhandisi Kundo amesema.
Amesema kazi hiyo ya kuunganisha mifumo ili isomane iharakishwe ikienda sambamba na ujenzi wa mfumo wa pamoja wa Dira za malipo ya kabla ya matumizi ( Universal Vending systems for Prepaid Water meter).
Amesema kiu kubwa ya viongozi ni kuona sekta inaondoka katika matumizi ya Dira za kawaida (mechanical meters )na kuingia katika matumizi ya Dira za malipo ya kabla (Smart Prepaid Meter) kama alivyoelekeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Lengo la mfumo ni pamoja na kuwezesha Dira za maji za kisasa (smart prepaid water meters) kufanya kazi kwa tja ili kuondokana na malalamiko ya wateja kudai kubambikiwa bili na kuepusha kiwango cha upotevu wa maji .
kwa kuanza kazi ya kuitengeneza mifumo yote katika wizara kusomana.