Maonesho ya fahari ya Geita awamu ya Tano ambayo yameanza kwenye Viwanja vya EPZA Bomba mbili Mjini Geita,yanatarajia kufunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela Siku ya Jumapili tar 26 Mei 2024.
Akizungumza na waandishi wa Habari mapema leo kwenye viwanja hivyo Mkuu wa Wilaya ya Geita,Hashim Komba amesema maonesho hayo yanakwenda kuwa na tija kutokana na kwamba yamegusa sekta mbalimbali ikiwemo ya kilimo,uvuvi pamoja na mitambo ya uchimbaji wa kisasa wa madini ya dhahabu.
“Naomba nitumie nafasi hii kuwashukuru sana waandaaji wa maonesho ya fahari ya Geita ,Kwanza nishukuru kwa uratibu ambao umekuwa ukifanywa kama tunavyojua serikali ya awamu ya sita imeendelea kuchochea maendeleo zaidi kwenye sekta ya viwanda,biashara pamoja na kilimo niwaombe sasa wananchi wafike na waje wajione namna bidhaa mbalimbali za viwanda ambazo zinaoneshwa zikiwemo pia bidhaa za kilimo ambazo zipo kwenye maonesho haya ya fahari ya Geita”Hashim Komba Mkuu wa wilaya ya Geita.
Aidha Komba ametoa Rai kwa wananchi waliopo Wilayani Geita na Mkoa wa Geita kufika kwenye maonesho hayo kwaajili ya kujifunza namna mambo mbalimbali pamoja na kujionesha bidhaa ambazo zimeletwa kwaajili ya wajasiriamali ambao wametoka nje ya Nchi na wengine mikoa mbalimbali.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chemba ya Biashara ,viwanda pamoja na Kilimo(TCCIA),Mhandisi Robert Gabriel ,amesema lengo kubwa la maonesho hayo ni kugusa sekta ya viwanda ,kilimo na ufugaji ambazo zimekuwa zikitumika kwa watanzania wengi.
“Kumekuwa na Mwitikio mkubwa sana kwa maana ya watu mbalimbali na makampuni tayari yameshafika kwaajili ya kushiriki maonesho zikiwemo bidhaa kutoka nje watu wakija kwenye maonesho tunaamini watapata fursa ya kuona vitu mbalimbali tayari na timu kutoka Zanzibar wameshafika kwaajili ya kushiriki maonesho yetu lakini pia ni fursa ya wao kuja kujifunza mambo mbalimbali ambayo yapo kwenye maonesho”Robert Gabriel Mwenyekiti wa TCCIA.