Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU) akifuatilia Mdahalo wa Viongozi mbalimbali katika maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza hilo uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.
…………………….
(John Bukuku na Sophia Kingimali)
Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amesema tangu kuanzishwa kwa baraza la amani na usalama la umoja wa Afrika limekuwa na nafasi muhimu katika kukuza amani, usalama na utulivu.
Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam leo Mei 25,2024 Jijini Dar es salaam katika maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika yaliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo marais wastaafu wa Afrika.
Amesema Tanzania itaendelea kuhakikisha umoja katika Baraza la Amani na Usalama wa Afrika, unakuwa madhubuti ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na baraza katika kutoa hamasa, kulindaa amani na kuhakikisha ustawi wa watu.
Rais Dk. Samia ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza hilo amesema ni muhimu kwa baraza kuwashirikisha vijana na wanawake katika kuimarisha na kuleta maendeleo ya kiusalama ili kuleta mabadiliko chanya pamoja na kuleta maendeleo kijamii na kiuchumi.
Amesema jitihada za pamoja ni muhimu katika kuimarisha usalama, hivyo ni muhimu kwa wanachama na baraza kwa ujumla kuongeza ushirikiano na wadau wa makundi mbalimbali.
Rais Dk. Samia akizungumzia miaka 20 ya baraza hilo, amesema kama ilivyokuwa enzi za Hayati Mwalimu Julius Nyerere, amewahakikishia Umoja wa Afrika (AU) kuwa Tanzania inafanya kila linalowezekana kuona unafikia malengo yaliwekwa na waasisi.
“Leo imetimia miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika. Baraza hili lina jukumu la kuzuia, kudhibiti na kutatua migogoro katika bara letu la Afrika hivyo niwapongeze viongozi wote kwa hatua tulifikia”,Amesema.
Rais Dk.Samia alizipongeza nchi wanachama wapya waliojiunga na baraza hilo kuanzia April, mwaka huu, hivyo aliwaahidi ushirikiano katika mambo yote ambapo nchi wanachama wa AU 53 kati ya 55 zimeridhia itifaki ya uanzishwaji wa baraza hilo.
AKIZUNGUMZIA KUNYAMAZISHA MITUTU
Rais Dk. Samia amesema Baraza hilo limekuwa lango na nafasi muhimu katika kukuza amani na ulinzi Afrika na bado linaendelea na jitihada za kutokomeza mitutu Afrika.
Amesema katika hatua za awali, ni muhimu kuimarisha mifumo ya utambuzi wa migogoro na kuzuia masula ya ugaidi na kuimarisha demokrasia na utawala bora.
Rais Dk. Samia amesema baraza la Amani na usalama Afrika limeweza kutembelea na kufanya ziara katika nchi ambazo zina migogoro na kuelewa vyema changamoto za nchi hizo, hivyo limeonesha mshikamano na wahusika wa migogoro kwa nia ya kuzuia na kuitokomeza kabisa.
Akizungumzia mafanikio Rais Dk. Samia ameainisha mafanikio ya baraza kuwa ni kuanzishwa kwa majadiliano baada ya vita, kukabiliana na migogoro na ugaidi, kujidhatiti kusimamia misingi ya haki za binadamu na ushirikiano wa taasisi.
Amesema ili kuimarisha amani na usalama Afrika, baraza linapaswa kuongeza uwezo wa kuzuia migogoro kwa kutumia nyenzo zilizopo, kuzuia migogoro isiwe endelevu kupitia mifumo ya utambuzi wa mapema, kuwepo kwa majadiliano na kuimarisha michakato ya maridhiano.
“Ipo mifumo ambayo haitumiki vizuri hivyo ni muhimu kuimarisha amani kutumia jeshi la Afrika, utekelezaji madhubuti wa nyenzo hii itasaidia kudhibiti mitutu,” amesema.
RAIS ATUNUKIWA TUZO
Pia Rais Dk. Samia ametunukiwa tuzo maalumu ya umahiri wa uongozi kutoka kwa Kamisheni ya Umoja wa Afrika(AU) iliyokabidhiwa kwake na Mwenyekiti wa kamisheni hiyo, Moussa Faki Mahamat.
Rais Dk. Samia amekuwa Mwenyekiti kwa Mei, ambapo Tanzania ni kati ya nchi 15 ambazo ni wajumbe wa baraza hilo, miongoni mwa nchi 55 wanachama wa AU.
Tuzo hiyo inatokana na kutambua umahiri wake katika uongozi na mchango katika masuala ya amani na usalama barani Afrika.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat amesema baraza linatekeleza majukumu yake kwa kufanya mabadiliko katika masuala ya amani ili kutekeleza wajibu wa waasisi wa bara la Afrika akiwemo Hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Amesema ni muhimu kila mwanachama kufuata kanuni na katiba za uanzishwaji wa baraza ili kuongeza ufanisi wake, kuleta demokrasia na utawala bora.
“Kuna nchi zinashindwa kufuata kanuni za baraza hili na kufuata kanuni za nchi zao hivyo kupuuza kanuni za baraza na kujikuta wakiingia katika migogoro mbalimbali,” amesema.
Amesema kupitia Baraza hilo wamefanikiwa kutatua migogoro mbalimbali ikiwemo nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Comoro, Sudani, Somalia na Ethiopia.
Ameainisha baadhi ya changamoto zinazoikabili baraza hilo kuwa ni uhitaji wa haraka wa kufanya tathmini ya uhuru kwa bara hilo, mabadiliko yasiyozingatia katiba kwasababu hayavumiliki.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza kwenye Mda
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi kutoka nchi mbalimbali kabla ya kuanza kwa mkutano wa kuadhimisha miaka 20 ya Baraza hilo uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.
Kikundi cha Vijana Wakitanzania kikitumbui
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU) akiwa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Mhe. Moussa Faki Mahamat pamoja na viongozi wengine wakati wakiangalia uzinduzi wa Nembo ya Baraza la Amani na Usalama wakati wa Maadhimisho hayo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassanambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU) akipiga makofi mara baada ya uzinduzi
wa Nembo ya Baraza hilo wakati wa Maadhimisho hayo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.
Rais Mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo akizungumza kwenye Md