Ofisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Kwimba, Emmanuel Katemi akitoaa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya elimu (bweni, maabara na vyumba vya madarasa 112) iliyogharimu milioni 501 kwa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Mwanza, leo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Michael Masanja ‘Smart’ akiandika ubaoni akimshukuru Rasis Dk. Samia kwa kuleta fedha za maendeleo wilani Kwimba, leo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Michael Masanja, akizungumza baada ya Kmati ya Siasa kukagua bweni la wasichana, Nyamilama Sekondari, leo.
…………
NA BALTAZAR MASHAKA, KWIMBA
SERIKALI kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA),imetumia sh.milioni 501 kukamilisha bweni la wasichana, maabara na vyumba vya madarasa ya Shule ya Sekondari Nyamilama wilayani Kwimba.
Ofisa Elimu Wilaya Kwimba,Emmanuel Katemi, amesema wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo kwa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Mwanza, leo.
Almeema serikali imejenga na kukamilisha bweni la wasichana 180 wa Shule ya Sekondari Nyamilama ili kuwaepusha na mimba za utotoni kwa sh. milioni 140, maabara mbili za Kemia na Baiolojia kwa sh.milioni 118.
Katunzi amesema katika kuchochea wanafunzi kujifunza imekamilisha miundombinu ya vyumba 112 vya madarasa kwa sh.milioni 240 zilizotolewa na serikali kupitia Mradi wa TEA.
“Kujengwa kwa miundombinu hii kumeleta manufaa kwa shule, mazingira yameboreka,ufaulu umeongezeka,mimba za utotoni zimepungua ari ya watoto wa kike kupenda masoo ya Sayansi imeongezeka,” amesema Katunzi.
Ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha za kuboresha sekta ya elimu kwa ujenzi wa miundombinu ya Sekondari ya Nyamilama ambayo imekuwa ikifanya vizuri kwa matokeo ya mitihani ya taifa ya kidato cha nne mkoani Mwanme.
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Michael Masanja ‘Smart’ amesema Kamati ya Siasa imefarijika kwa utekelezaji bora wa Ilani ya Uchaguzi Nyamilama sekondari.”Kamati imekuja kuagalia kilichofanyika kwa fedha alizoleta Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, tullichokiona kinalingana na thamani ya fedha, shule hii ni nzuri kwa mazingira ya kujifunzia na kufundishia baada ya Dk.Samia kuibadilisha, ni shule bora kuliko za binafsi,”amesema
Smart amesema penye ushirikiano mambo yana kwenda vizuri na mafanikio yanaonekana , hivyo kamati imeridhika kwa kazi zilizofanyika Kwimba na kuwahimiza kuendelea kuchapa kazi ili kuleta matokeo chanya katika kuleta maendeleo ya jamii.