Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene, mapema asubuhi ya leo 24.05.2024 amefanya ziara ya kutembelea mradi wa Nyumba za Makazi zilizojengwa na Watumishi Housing Investments (WHI) katika eneo la Isangijo, Kisesa Mkoani Mwanza.
Baada ya kutembelea mradi huo Mhe.Simbachawene ameipongeza WHI kwa kutekeleza mradi huo wenye jumla ya Nyumba 59 ambapo nyumba 20 zimenunuliwa na nyumba 39 kupangishwa kwa watumishi wa Umma.
Aidha Mhe.Simbachawene ameagiza kuendelea kutafuta viwanja katika maeneo mbali mbali Nchini kwa kusjirikiana na mamlaka husika maeneo hayo ili kutimiza lengo la Taasisi hiyo ambalo ni kutoa huduma ya Makazi Bora na kwa Bei nafuu kwa Watumishi wa umma, wafanyakazi wa sekta binafsi pamoja na wanachama wote wa mifuko ya hifadhi ya jamii.