Serikali ya Tanzania inaendelea kutekekeleza mikakati ya kujitosheleza za kwa mbegu za mazao ya kilimo ili kuihakikishia nchi usalama wa chakula pamoja na fursa za kibiashara.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe (Mb) tarehe 24 Mei 2024, alipofungua Mkutano wa Wadau wa Tasnia ya Mbegu uliofayika jijini Dodoma.
Mhe. Bashe amewataka wadau wa tasnia ya mbegu kushirikiana na seeikali katika uzalishaji wa mbegu ili kupunguza uagizaji wa mbegu za mazao kutoka nchi za nje.
Aidha, Mhe.Bashe ameziagiza taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Kilimo ambazo zinamiliki mashamba ambayo hawayatumii kutoa ardho hizo kwa sekta binafsi ili waweze kuzalisha mbegu.
Waziri Bashe amewahakikishia wadau mbegu kuwa serikali inaunga mkono uhifadhi na uendelezaji wa mbegu za asili.
Mhe. Bashe amewaasa wazalishaji wa mbegu kuwa na chombo kimoja ambacho kitawaunganisha katika umoja wao ili kurahusisha mawasiliano kati ya yao na serikali.