Wakati Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ikiendelea kuifungua Nchi kimataifa,matokeo ya kumiminika Kwa wawekezaji yameendelea kuonekana, baada ya uzinduzi wa hotel kubwa na ya kifahari ya ” KingJada Hotel ” iliyopo katika mradi wa Morocco Square chini ya National Housing Corparation
( NHC )
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo
meneja wa hoteli hiyo Adeline Mmasi amesema juhudi za serikali katika kuwalinda na kutoa fursa za uwekezaji ndio zimepelekea kufanikisha uwepo wa hoteli hiyo ya kisasa
” Tunamshukuru Rais Samia kwa kutoa fursa kubwa Kwa upande wa utalii,kwamaana na sisi tumepata nafasi ya kuweza kufungua sehemu mpya,ambapo tunawakaribisha Watanzania na wageni kutoka nje ya Tanzania,huku lengo letu kubwa likiwa ni kutoa ajira Kwa vijana na watu wote kadri itavyowezekana ” Alisema meneja huyo.
Naye Kaimu Meneja Mauzo na masoko kutoka NHC Emmanuel Lyimo amesema Shirika limekuwa likizingatia mazingira mazuri ya uwekezaji hivo amewasihi wawekezaji wazidi kuja Kwa wingi ili Kuwekeza
” Sisi kama NHC tumeandaa mazingira mazuri ya uwekezaji ndio maana tumekuja na mradi huu wa morocco square. Tunajivunia kupata mwekezaji KINGJADA HOTEL ambaye amewekeza kwenye hotel iliyojengwa na shirika la nyumba la Taifa ” alisema meneja huyo Emmanuel
Naye Meneja Rasilimali Watu wa hotel ya KingJada Yohana Mwaigaga amesema tayari watanzania zaidi ya 100 wamepata ajira katika hoteli hiyo
” Tumeajiri Watanzania zaidi ya 100 ambao wamenufaika na ajira katika yetu kutika idara tofauti ” alisema meneja huyo.