Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma Jaji Mstaafu Sivangilwa Mwegesi akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam katika kikao kazi na Sekretarieti hiyo kilichofanyika kwenye ukumbi wa BoT.
Katibu Ukuzaji Maadili Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw.Waziri Kipacha kushoto na Bw. Honoratus Ishengoma, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Sejretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma wakiwa katika kikaokazi hicho.
KATIBU Ukuzaji Maadili Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw.Waziri Kipacha akijibu baadhi ya maswali ya wahariri wa vyombo vya habari.
Johanither Barongo ,Afisa habari Mkuu akifafanua jambo katika kikaokazi hicho.
Omary Juma, Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini akiwasilisha mada katika kikaokazi hicho.
…………………….
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma Jaji Mstaafu Sivangilwa Mwegesi ametoa rai kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini kuibua changamoto ambazo zinakwamisha uadilifu kwa viongozi na watumishi wa umma.
Wito huo ameutoa leo Mei 24,2024 jijini Dar es salaam wakati wa kikao kazi kati ya wahariri wa vyombo vya habari na Sekretarieti hiyo.
Amesema Sekretarieti pekee haiwezi kutoa elimu uadilifu peke yake bila msaada wa wadau wengine hasa vyombo vya habari kwani vinauwezo wa kufika mbali na kuwafikia watu wengi zaidi.
“Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma pekee yetu hatuwezi kutoa elimu ya uadilifu bila msaada wa wadau wengine mkiwemo nyinyi wahariri ambao vyombo vyenu vina sauti kubwa ya kuweza kufika mahali popote hapa nchini kwetu”,Amesema.
Aidha Kamishna amesema uadilifu wa viongozi na watumishi wa umma ukiongezeka utasaidia kukuza maendeleo ya Taifa na kuongeza imani ya wananchi kwa serikali.
“Niwaombe kutumia karamu zenu muandike makala nyingi za kuelezea maadili kwa watumishi wa umma ili kuwaondolea viongozi na wananchi hofu pindi tunapotimiza wajibu wetu”,Amesema na kuongeza.
“Ndugu wahariri naviasa na kuviomba vyombo vya habari vijikite katika kujenga hoja ,kuchapisha na kutangaza habari linganifu zilizosheheni ukweli bila uonevu”,Amesema.
Akizungumzia kuhusu maadili kuelekea uchaguzi wa Serikali ya mtaa ma uchaguzi Mkuu 2025 Kamishna amesema viongozi wanapaswa kuzingatia taratibu na kanuni za uchanguzi zilizowekwa.
“Tunapofikia kipindi cha uchaguzi watu wengi wanapenda kutumia njia ya mkato kujipatia kura niwasihi wawe waadilifu lakini pia vyombo vya habari mnapaswa kutumia vyombo vyenu kuhakikisha mnaelezea kuhusu uadilifu ili kuwafikia watu wengi zaidi”,Amesema Jaji Mwangesi.