Serikali imesema itaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya Rujewa –Madibira hadi Mafinga yenye urefu wa
kilometa 151.1 ili kurahisisha shughuli za kiuchumi na maendeleo wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godifrey Kasekenya ameyasema hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali
la mbunge wa jimbo la Mbarali na kusisitiza kuwa nia ya serikali ni kuhakikisha inakamilisha ujenzi huo kadri ya upatikanaji wa
fedha
“Mh.Spika nikuhakikishie adhma ya Serikali ni kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo ili kuleta maendeleo kwa wananchi wa wilaya ya Mbarali ambao eneo lao lina uzalishaji mkubwa wa mazao , na hivyo kukuza uchumi wa wananchi na Taifa kwa
ujumla,”Amesema Kasekenya
Aidha taratibu za manunuzi kwa ajili ya kumpata Mkandarasi wa ujenzi kwa sehemu ya Igoma hadi Kinanyambo A Km 52.2
zinaendelea ambapo mkataba unatarajiwa kusainiwa mwisho ni wa mwezi juni 2024.
Mh. Mbunge wa jimbo la Mbarali Bahati Ndingo alitaka kujua ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa barabara ya Rujewa-Madibira hadi Mafinga kwa kiwango cha lami.