NA BALTAZAR MASHAKA, MISUNGWI
UONGOZI wa Shule mpya ya Msingi Shilabela,wilayani Misungwi, umeipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuboresha sekta ya elimu ikiwemo kujenga miundombinu ya madarasa na matundu ya vyoo na kununua samani.
Amesema shule hiyo yenye wanafunzi 1,035 imejengwa na serikali mwaka 2022/23 ili kupunguza msongamano wa watoto katika Shule ya Msingi Mbela yenye wanafunzi 2,610 huku mundombinu ikiwa haikidhi mahitaji.
“Tunaipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan,kwa kuboresha sekta ya elimu ya msingi,ameleta fedha za kujenga jengo la utawala la shule ya Shilabela,ofisi 4 za walimu,madarasa 16,matundu 27 ya vyoo vya wanafunzi wa awali,msingi na walimu,”amesema.
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza,Michael Masanja ‘Smart’ kwa niaba ya Kamati ya siasa baada ya kukagua mradi huo wa BOOST amesema,Rais Dk.Samia na serikali yake amefanya kazi kubwa ya kuboresha elimu husasani ujenzi wa miundombinu na ununuzi wa samani.
“Zimeletwa fedha nyingi za uboreshaji wa elimu mkoani kwetu (Mwanza),zimetoka kwa Dk. Samia hivyo wanafunzi watambue kuwa Rais huyo wa Awamu ya Sita anawapenda na ameridhia kuwaletea fedha za kuboresha miundombinu ya elimu,haya tulizoea kuyaona shule binafsi leoe amebadilisha hali hiyo,”amesema.
Samrt amekiri madarasa hayo ya mradi wa BOOST yamejengwa kwa kiwango cha ubora na akatoa rai kwa wanafunzi kusoma kwa bidii wafaulu kwa kiwango cha juu kuifanya shule ya mfano pia,waitunze miundombinu hiyo idumu kwa kizazi cha ssa na vijavyo.
Awali kamati hiyo ilikagua na kuridhishwa na mradi wa mabweni mawili ya wasichana Misungwi Sekondari yaliyogharimu sh.milioni 192
“Niwapongeze kwa usimamizi mzuri wa fedha za miradi hii ya mabweni ya wasichana,rai yangu someni kwa bidii na kufaulu kwa daraja la kwanza,ukosefu wa umeme hilo litashughilikiwa watoto wasome hata usiku,”alisema Smart na kuahidi kuwapelekea Luninga wapate taarifa na kufahamu yanayofanywa na serikali yao.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Shule hiyo, Alnold Rwiza bweni moja limekamilika kwa sh. milioni 62 litachukua wanafunzi 94 na jingine linalojengwa kwa sh. 129 wanatarajia kuchukua wanafunzi 194, lengo ni kuboresha mazingira ya kujifunza na kufundishia,changamoto ni kutounganishwa na nishati ya umeme.