Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mkoani Dar es salaam Jaffar Juma Nyaigesha akizungumza na kuongoza kikao muhimu cha kawaida cha Baraza la Madiwani ambacho kimefanyika leo Mei 23,2024 kwenye ukumbi wa Manispaa hiyo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mkoani Dar es salaam Aron Kagulumjuli akizungumza katika kikao muhimu cha kawaida cha Baraza la Madiwani ambacho kimefanyika leo Mei 23,2024 kwenye ukumbi wa Manispaa hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Uchumi,Afya na Elimu Joseph Thomas Kleruu akiwasilisha taarifa ya kamati yake katika kikao muhimu cha kawaida cha Baraza la Madiwani ambacho kimefanyika leo Mei 23,2024 kwenye ukumbi wa Manispaa hiyo.
Diwani wa Kata ya Makurumla Bakari Kimwanga akichangia ajenda iliyokuwa ikijadiliwa katika katika kikao muhimu cha kawaida cha Baraza la Madiwani ambacho kimefanyika leo Mei 23,2024 kwenye ukumbi wa Manispaa hiyo.
Baadhi ya madiwani wa Manispaa ya Ubungo Mkoani Dar es salaam ambao wamehudhuria katika katika kikao muhimu cha kawaida cha Baraza la Madiwani ambacho kimefanyika leo Mei 23,2024 kwenye ukumbi wa Manispaa hiyo.
Baadhi ya watendaji wa Manispaa ya Ubungo Mkoani Dar es salaam ambao wamehudhuria katika katika kikao muhimu cha kawaida cha Baraza la Madiwani ambacho kimefanyika leo Mei 23,2024 kwenye ukumbi wa Manispaa hiyo.
………………………
NA MUSSA KHALID
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Mkoani limemtaka Meneja wa TARURA katika Manispaa hiyo kuhakikisha anakutana na Madiwani na watendaji wa manispaa hiyo ili kueleza mpango wa ukarabati wa miundombinu ya barabara katika kata na mitaa yote kufuatia barabara nyingi kuharibika kutokana na mvua kubwa zilizonyesha katika mkoa wa Dar es Salaam
Hayo yamejiri leo katika kikao muhimu cha kawaida cha Baraza hilo cha robo ya tatu ya mwaka katika kipindi cha mwaka 2023/2024 ambacho kimeongozwa na Mwenyekiti na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Jaffar Juma Nyaigesha sambamba na Katibu wake Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Aron Kagulumjuli ambapo imejadiliwa na kupitishwa ajenda mbalimbali.
Akizungumza wakati akifungua Kikao hicho Mastahiki Meya wa Ubungo Nyaigesha amemtaka meneja wa TARURA kuhakikisha wakandarasi wao wanaboresha utekelezaji wa barabara hizo ili kuweza kuwaondolea adha wananchi.
‘Ni lini Meneja atakuatana na waheshimiwa madiwani ili awaelezee mipango na changamoto zote za miundombinu ya barabara kwani zote ni madimbwi hivyo tunamtaka aje kuzungumza nao’amesema Meya Nyaigesha
Aidha Meya Nyaigesha amemtaka Mhandisi Mwandumya ambaye amemwakilisha Meneja wa TARURA kufikisha salamu hizo za waheshimiwa ili jambo hilo liweze kupatiwa utatuzi wa haraka.
Akizungumza kwa niaba ya Meneja wa TARURA Ubungo,Mhandisi Emanuel Mwandumbya amesema tayari baadhi ya barabara wamekwisha zitangaza na zitaanza kufanyiwa matengenezo mwanzoni mwa mwezi sita mwaka huu.
‘Kuna barabara mbili za vumbi ambazo zinaenda kutangazwa mwanzoni mwa mwezi wa sita tayari zipo mpango na mwezi wa saba kwa ajili ya matengenezo’amesema Mhandisi Mwandumbya
Kwa upande wao baadhi ya madiwani wa Baraza hizo akiwemo Diwani wa Kata ya Kwembe Nicholas Batalingaya ,Diwani wa Kata ya Makurumla Bakari Kimwanga pamoja na Diwani wa Kata ya Msigani Hassan Mwasha wameisihi TARUTA kufika katika kata zao na kujionea changamoto ambazo wananchi wao wanakumbana nazo kutokana na miundombinu hiyo kuharibiwa na mvua.
Hata hivyo Baraza hilo pia limetumia fursa hiyo kumpongeza mkuu wa wilaya ya Ubungo Hassan Bomboko pamoja na watumishi wote wa wilaya ya Ubungo kwa kufanikisha kukimbiza mbio za Mwenge 2024 kwa kishindo katika wilaya ya Ubungo na kuweza kupitisha jumla ya miradi yote nane