Kampuni ya Heineken Inatarajia kuzindua rasmi jarida lake jipya la vinywaji ikiwa ni siku chache baada ya kununua rasmi kampuni ya Distell na kampuni ya bia ya Namibia (NBL).
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 22,2024 Jijini Dar es salaam Meneja mkaazi wa kampuni ya HEINEKEN, Obabiyi Fagade amesema uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika mei 25,jijini hapo ambapo mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa nchi,Ofisi ya Rais,Mipango na uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo ambapo atajumuika na viongozi kutoka tasnia mbalimbali.
Amesema kwenye jarida hilo ambalo linafanya kazi chini ya jina la HEINEKEN litaonyesha dhamira ya kampuni ya kuhakikisha inaendelea kusambaza vinywaji vyenye ubora wa hali ya juu kwa uatumiaji.
“Ununuzi wa kampuni hizi unaongeza zaidi ya Euro bilioni 1 katika mapato halisi lakini inaongeza Euro milioni 150 katika faida ya uendeshaji hivyo tunaamini kwa uendeshaji ambao tunao hapa nchini utasaidia kwa kiasi kikubwa katika kukuza uchumi hapa nchini”,Amesema Fagade.
Aidha ameongeza kuwa uwepo wa kampuni hizo hapa nchini utasaidia kuongeza ajira kwa wananchi wengi hasa vijana.
Kwa upande wake Meneja biashara na Masoko Lilian Pascal amesema wamejipanga kuhakikisha wanatoa huduma zenye ubora wa kiwango cha juu.
Amesema wamejipanga kuwa kiongozi wa soko katika tasnia ya vinywaji nchini kwa kufuata kanuni na maadili yake ya msingi.
“HEINEKEN sasa inapatikana katika masoko 114 lakini inauzwa kwa zaidi ya masoko 180 hivyo tupo tayari kuwa kiongozi wa soko katika tasnia hii ya vinywaji tumejitolea kutengeneza nafasi za furaha kwa wateja wetu kwa kutumia ubunifu na ufanisi wetu katika kutoa huduma”,Amesema Lilian